28.11.12

"FASTJET" NDEGE YA SH.32,000/= KUANZA SAFARI RASMI




Bwana  Charles Tizeba ,(Naibu Waziri wa Uchukuzi) akizindua safari za ndege za Kampuni ya Fastjet jijini Dar es Salaam jana, alisema kuwa kuanzishwa kwa safari za ndege za bei rahisi kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza kunatoa changamoto kwa Serikali kuboresha miundombinu kukidhi mahitaji ya ongezeko la wasafiri.
PIA aliongeza kwa kusema "Kuanzishwa kwa safari za ndege za bei rahisi ya Sh 32,000 na Kampuni ya Fastjet kunatarajiwa kuvutia abiria wengi zaidi, hali ambayo viwanja vingi nchini vikiwamo vya Mwanza na Kilimanjaro haviwezi kutimiza mahitaji,
KUTOKANA na hilo ameagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuandaa mazingira mazuri na miundombinu katika Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro kukabiliana na ongezeko la abiria wanaotarajia kuvitumia.