18.5.13

Vugugu la uchaguzi SUA,wagombea tumbo joto....




 Ikiwa ibaki siku moja tuu baada ya wanachuo woote wa sua kuchagua  uongozi mpya, kuongoza kwa kipindi cha muhula mwingine tena wagombea wanaogombea nafasi mbalimbali wakiwa tumbo joto kila mmmoja kuomba ashinde nafasi aliiomba kuchaguliwa.

Hili litawezekana kwa upande mmoja tu wa shilingi kushika hatamu kwa kipindi kingine kinachokuja.

Hapo ikiwa kesho ndio itakuwa siku maalumu kwa wanafunzi woote wa sua kuamua nani atawaongoza katika kipindi kingine cha mwaka mmoja.

Wagombea mbalimbali wamenadi sera zao na leo ndio siku ya mwisho wa kampeni hizo ,hivyo leo ni kampen za lala salama yaani leo(jumamosi,18/05/2013) ndio mwisho kwa kila mdogombea kunadi sera zake.

Nafasi zinanzo gombewa kwa mujibu wa katiba ya Sokone University of Agriculture Students organization
 ( SUASO) ni Rais akiwa pamoja na mmgombea mweza wake(Makamu wa Rais),na wabunge ambao wabunge itakuwa ni baada kupatikana kwa rais na makamu wake.

Wagombea hao ni ANDREW ZIRACK ( Akiwania Urais ) akiwa na mgombea mwenza  SHOO LERNARD (Makamu wa rais), MSEMEMBO BERNARD (akiwania Urais), mgombea mwenza wake ni IRENE MASANGWA (Makamu wa Rais), na GEORGE, LENA (Akiwania Urais) akiwa na mgombea mwenza MSEMO, OBADIA (Makamu wa rais).

Kazi itakuwa kesho kwa kila mwanasua kumchagua mgombea anyefaa kuongoza, maana uchaguzi una sehem kuu mbili kampeni na kuchagua, na kwa tathmini kampen zimeenda vizuri kwa kila mgombea kupata nafasi ya kujinadi kazi kesho ni kila mmoja wetu kwa pamoja tupiga kura kufanya uchaguzi wetu kwa utulivu.

Sababu kumekuwa na mahudhurio machache ya kwa wapiga kura kuhdhuria ktk upigaji kura lakin hili pia ni tatizo la nchi kwa ujumla,wito wangu kwa wanchuo wenzangu kuhudhuria kwa wingi katika zoezi la uchaguzi wa SUASO GORVENMENT LEARDERS.

"TOGETHER WE CAN MAKE CHANGES AT SUA !..............."