28.11.12

POLISI TENA WAUA MTU KWa KISU



Watu 10 wanaodhaniwa kuwa ni askari wa (JWTZ) Jeshi la Wananchi Tanzania kikosi cha 44 KJ 

 Kambi ya mji mdogo wa Mbalizi  wanashirikiwa na polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya 
mkazi wa mji huo, Petro Sanga. 
Askari hao wanadaiwa kumuua Sanga kwa kumchoma kisu 
shingoni na mdomoni, kisha kuwajeruhi watu wengine sita kwenye Baa iitwayo Power Night, ambako walikwenda kwa lengo la kulipiza kisasi cha kupigwa kwa askari mwenzao, Geodfery Matete.
Uhalifu huo wa mauaji hayo yamekuja siku moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar  es Salaam  kuwahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa askari  watatu wa JWTZ na JKT, baada ya kupatikana  na hatia ya kumuua, Swetu Fundikira.Hivyo, askari hao waliohukumiwa kunyongwa, jana waliwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika  Mahakamani hapo.