Pichani ni mmoja wa Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mkoa Singida, akijaribe kurekebisha mapambo ya jeneza lililokiwa na mwili wa marehemu Munchari Lyoba,baada ya kuharibiwa
Majambazi, wamevamia
gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka mjini Morogoro kwenda mkoani Mara
kisha kupora fedha pamoja na vitu mbalimbali vyenye dhamani ya takriban
Shilingi milioni 19 za kitanzania,Ni fedha na vitu walivyokuwanavyo
waombolezaji.
Tukio hilo la kusikitisha lililotokea juzi
mkoani Singida, majambazi hao walivunja vioo vyote vya gari pamoja na
jeneza lililokuwa na mwili wa Munchari Lyoba aliyekuwa mwanafunzi wa
mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) cha Morogoro na kumpekua
marehemu.
JANA akizungumza na
waandishi wa habari nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa
Singida, mkuu wa msafara uliokuwa ukisafirisha maiti, Makaranga alisema
kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 7:30 usiku katika gari aina ya Land Cruiser
mali ya SUA.
WAKATI akisimulia
tukio hilo, Makaranga alisema kuwa lilitokea katika Barabara Kuu ya Dodoma –
Mwanza nje kidogo ya Mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed
Trans kuelekea mkoani Mara.
Alisimulia kwamba gari
hilo pamoja na jeneza, lililobeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi
wengine wanne lilipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa
barabarani na kuwalazimisha kusimama ndipo wakavamiwa na kundi kubwa la vijana,
ambao walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.
“Walipofika walipiga
kioo cha gari letu kwa mbele na kumparaza kwa panga usoni dereva wetu.
Baada ya hapo walivunja vioo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu tulichokuwa nacho,” Makaranga akisimulia.
Baada ya hapo walivunja vioo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu tulichokuwa nacho,” Makaranga akisimulia.
Pia Makaranga
aliongeza kwa kusema, kuwa katika tukio hilo, aliporwa Sh2 milioni
alizokabidhiwa azihifadhi kwa ajili ya kugharimia msafara huo, Sh8.8 milioni
zilizochangwa na wanafunzi kama rambirambi kwa mwenzao na jumla ya
Sh9 milioni ambazo wasindikizaji walikuwa nazo mifukoni mwao.
“Pia tuliporwa simu
zetu zote za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu,”
alisema.
Makaranga aliyeeleza
kuwa anafanya kazi za kiutawala SUA, aliwataja walioumizwa na majambazi hao
kuwa ni pamoja na yeye, dereva wao na kiongozi wa wanafunzi, Idd Idd ambao
walitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na kuruhusiwa.
Mkuu wa Wilaya ya
Singida, Mwalimu Queen Mlozi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza
kuwa amewasiliana na uongozi wa SUA ili watume gari lingine na kukarabati jeneza
lililoharibiwa na majambazi hao.
Mlozi aliongeza kuwa
kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi na Kamati ya Ulinzi na Usalama,
watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa haraka iwezekanavyo ili
waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
“Tukio hili limenisikitisha sana, maana sasa binadamu wametokwa na utu wa ubinadam kwenye akili zao na kuhamia kwenye vitendo ambavyo si vyakiungwana kabisa na kamwe hawezi kuthubutu kuvifanya mtu mwenye akili timamu na utu, maana watu wanapekua hadi maiti na kuisachi!".
“Tukio hili limenisikitisha sana, maana sasa binadamu wametokwa na utu wa ubinadam kwenye akili zao na kuhamia kwenye vitendo ambavyo si vyakiungwana kabisa na kamwe hawezi kuthubutu kuvifanya mtu mwenye akili timamu na utu, maana watu wanapekua hadi maiti na kuisachi!".