Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia waziri wa nchi,
ofisi ya waziri mkuu,sera na uratibu bungeni, Msh.William Lukuvi, imetangaza
uamuzi wa kupanga upya matokeo ya kidato cha nne ya 2012. Ukitangaza uamuzi huo mapema leo bungeni na Msh. William
Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu. Uamuzi umetokana na kamati ya waziri mkuu
iliyokuwa inachunguza kuhusu matokeo hayo kubaini kuwa matokeo hayo yalipangwa
kwa utaratibu tofauti na uliokuwa unatumika zamani.
WAKATI hapo awali taarifa zisizo rasmi zilieleza kwamba
matokeo hayo yalipangwa kwa kuzingatia madaraja haya hapa chini, japo Baraza la
Mitihani lilikanusha baadaye kwa kusema kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli:
A = 80%-100%-
B = 65%-79%-
C = 50%-64%-
D = 35%-49%-
F = 0%-34%-
Wakati huo tume ya Waziri Mkuu imebaini kutumika kwa
madaraja tofauti na uataratibu wa awali. Hivyo basi, matokeo yaliyotangazwa
hayatatumika tena mpaka yaje yaliyopangwa upya.