2.5.13
JAY DEE: WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE
28.4.13
PADRI AZIKWA AKIWA MZIMA
Tukio hilo limetokea katika Kitongoji cha Maweni kijijini hapo wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Mbeya. Msaidizi wa zamani wa Padri (Katekisita) katika
Kigango cha Kanisa Katoliki Kijiji cha Mkwajuni, Florian Mwamosi (70) amekufa
baada ya kuzikwa akiwa hai katika kaburi moja na mtu anayedaiwa kumuua kwa njia
ya kishirikina.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alikiri kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa lilitokea saa 9:00 mchana katika kijiji hicho cha
Maweni Mkwajuni wilayani Chunya.
“Marehemu aliuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa
na mawe kwa tuhuma za kuhusika na uchawi na kusababisha kifo cha Peter Robert,”
alisema.
Kamanda Athumani alisema kuwa uchunguzi kuhusiana na tukio
hilo unaendelea na kwamba wahusika wote wa tukio hilo wamekimbia na kuzihama
nyumba zao, hivyo polisi wanaendelea na msako wa kuwatia mbaroni watuhumiwa na
kwamba tayari kaburi hilo limefukuliwa
jana kutenganisha maiti hizo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa marehemu huyo ambaye alikuwa akituhumiwa kwa
ushirikina aliwahi kuwa Katekista wa kigango hicho hadi mwaka 2007.
Wameeleza kuwa Mwamosi alikwenda kuhudhuria mazishi ya
Peter Robert (28) katika kitongoji hicho
cha Maweni, baada ya kufuatwa nyumbani kwake na watu wakitaka aende kwa sababu
yeye ni mmoja wa wazee wa mila katika kitongoji hicho.
“Bwana Mwamosi alikuwa akituhumiwa kwa uchawi kwa muda mrefu
na wenzie wawili, hivyo alipofika makaburini ilianza minong`ono ya watu na huku
wengine wakiguna na ndipo alipoombwa aingie kaburini kwa ajili ya kupokea
jeneza lililobeba mwili wa marehemu Peter Robert,” alisema mkazi mmoja wa
kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Joseph.
Alisema kuwa baada ya kuingia kaburini akiwa na watu wengine
watatu wenzake walitoka kwa haraka na kumwacha Mwamosi peke yake ndipo kundi la
watu waliokuwa eneo hilo la makaburi walianza kumshambulia kwa kumpiga mawe
huku wakimwamuru akae chini.
Shuhuda huyo alisema kuwa baada ya kukubali kukaa chini
akiwa ndani ya kaburi hilo, walianza kumfukia na alipofukiwa nusu ya mwili wake
waliingiza jeneza la marehemu Peter na kuliweka juu yake na kuanza kulifukia
kaburi hilo.
“Baada ya kukaa chini ndani ya kaburi hilo ndipo walianza
kumfukia kwa udongo na baadaye wakachukua jeneza la marehemu na kuliweka juu
yake, kisha kumfukia na udongo na taratibu za mazishi ziliendelea kwa ajili ya
marehemu Peter,”alisema.
Alidokeza kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu Robert
kuugua ghafla tumbo, ndipo ndugu zake walipoamua kumpeleka kwa mganga wa jadi
kwa ajili ya kupata matibabu na baada ya siku tatu alifariki dunia.
TANZANIA INATENGA BILION 1 KILA MWAKA KWAAJIRI YA MAZISHI YA VIONGOZI KITAIFA
Fedha hizo ni zile zilizolalamikiwa na wabunge wakati wa
uwasilishwaji wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika pamoja na ile ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Kutokana na kuwapo mvutano mkali bungeni, kwa nyakati
tofauti Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, walilazimika kutoa maelezo ya
kina kuwashawishi wabunge wakubali ili fedha hizo ziidhinishwe katika bajeti
husika kwa ajili ya matumizi ya mwaka mpya wa fedha unaoanza Juni mwaka huu.
Fedha hizo ni Sh74 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mfuko
wa pembejeo, Sh1 bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi wa kitaifa, Sh88
bilioni za Ruzuku ya Mfuko wa Pembejeo na Sh29 bilioni kwa ajili ya kufuatilia
utekelezwaji wa miradi ya Serikali.
Baadhi ya wabunge walilalamikia fedha hizo wakisema kuwa ni
ulaji kwa wakubwa.
Wakizungumza na gazeti hili, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT),
Profesa Tolly Mbwete alisema kwa kuwa Bajeti ya Wizara ya Fedha itapitishwa
mwishoni, wabunge wanatakiwa kuikataa hadi mambo muhimu katika bajeti
zilizotangulia kusomwa, yatakapofanyiwa kazi.
“Binafsi naona hiyo ndiyo njia nzuri iliyobaki, wabunge
wanatakiwa kuamua mambo kwa masilahi ya taifa na siyo kwa manufaa na maslahi
yao binafsi,” alisema Profesa Mbwete.
Aliwataka wabunge kutumia fursa hiyo kumbana Waziri wa Fedha
ili kuhakikisha kuwa fedha zaidi zinaongezwa, au kupunguzwa katika maeneo
mengine, kwa ajili ya kupelekwa katika maendeleo.
Profesa Humphrey Moshi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM),
alisema kuwa fedha zaidi zinatakiwa kuongezwa katika bajeti ya maendeleo,
badala ya matumizi ya kawaida.
Aliongeza pia kwa kusema“Maendeleo yatapatikana kwa haraka kama tutawekeza zaidi ya
asilimia 20 ya bajeti yetu kwenye matumizi ya maendeleo. Hii ni tofauti na
sasa, ambapo asilimia 90 ya fedha zinazotengwa zinakwenda katika matumizi ya
kawaida,” .
12.4.13
NJOO SUA UJIONEE PANYA WANAVYOPATA MAFUNZO MPAKA WANAPATA DEGREE
Panya wanapata shule kuweza kutambua vitu mbalimbali kama vile mabomu yaliofukiwa ardhini,vimelea ya magonjwa kama vile TB na vitu vingine kuwafanya wanakuwa jasiri, mpaka anahitimu nakupatia chet hadi anafikia ktk shahada ya kwanza yaani degree. angalia hiyo video chini hapo utaona
18.2.13
MATOKEO KIDATO CHA NNE HAYA HAPO KWA URAHIS KABISA
Kwanza tumia MOZILLA FIREFOX BROWSER KUTAFUTIA MATOKEA ALAFU FUATA KWA KUBOFYA CHINI HAPO KATIKA HIYO LINK
http://www.moe.go.tz/examresults/olevel.htm
au
tumia hii kama hiyo haifunguki
http://webcache.googleusercontent.com/search?q=cache:http://196.44.162.25/necta2012/olevel.htm
http://www.moe.go.tz/examresults/olevel.htm
au
tumia hii kama hiyo haifunguki
http://webcache.googleusercontent.com/search?q=cache:http://196.44.162.25/necta2012/olevel.htm
13.2.13
WAZIRI ASEMA, MAKAHABA WOOTE WAPEWE VITAMBULISHO
Aminiata Toure ,Ambaye
ni waziri wa Haki nchini Senegal, amependekeza makahaba wote nchini humo wapewe
vitambulisho maalum.Alisema wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa kongamano muhimu
wiki ijayo kuhusu sheria za ukahaba.
Toure alisisitiza kuwa kadi hizo zipewe tu wanadada
waliozidi miaka 18, na watakaokiuka hilo wakamatwe na kushtakiwa.Vitambulisho
vimekuwa vikitolewa bila malipo kwa makahaba tangu miaka 20 iliyopita lakini
kwa machangudoa wanaoendesha biashara yao mjini Dakar na mitaa viungani.Waliopewa
kadi hizo walichunguzwa vikali na walihitaji kila mwezi kupita kipimo cha
HIV/Ukimwi ama maambukizi mengine ya zinaa.Waliokuwa wanaishi bila maradhi walitakiwa kutoa damu iliyowekwa
katika hifadhi na kupewa hospitali.
Waliopatikana na maambukizi madogo walitibiwa na kuruhusiwa
kwenda, na waliopatikana kuwa na vijidudu vya maambukizi walitengwa kando.Juhudi
hizo za tangu miaka ya mapema ya themanini kuhamasisha umma kuhusu janga la
ukimwi, zinaaminika kupelekea Senegal kuwa miongoni mwa mataifa yaliyo na
kiwango cha chini sana cha maambukizi ya HIV barani Afrika.
Lakini kongamano hilo la Jumatano linanuia kung’oa watoto
katika biashara hiyo na kuweka msingi wa sheria zenye uhalisi, kali na thabiti
na mikakati ya kudhibiti ukahaba nchini Senegal.Waziri huyo pia alipendekeza kikosi maalum kilichoundwa
kuwafuatilia mahakaba kipewe vifaa vya kutosha na vizuri vya kuwawezesha
kutekeleza jukumu hilo.
ALISEMA waziri huyo, “kudhibiti vyema ukahaba nchini
Senegal, twahitaji ushirikiano wa wadau kadha kama viongozi wa kidini na muhimu
zaidi wadau katika sekta ya utalii na burudani.”
Subscribe to:
Posts (Atom)