28.5.13

DIAMOND NA NEY KTK SHOW YA NEW MAISHA, ILIKUWA BALAA, CHECK IT DOWN



MSANII NGULI WA BONGO FLAVA ( MAGWEA ) AFARIKI DUNIA.



 Msanii nguli wa miondoko ya hip hop hapa nchi maarufu kama ALBERT MANGWEA, maarufu  kwa jina la NGWEA au MANGWEA amefariki duania akiwa huko AFRIKA KUSINI.Habari kutoka kwa rafiki yake wa karibu alipofikia zinasema kuwa MANGWEA alirud kutoka matembezini na kulala,

kilichowashangaza zaid ni kulala kwa mda mrefu wakati alikuwa na safari ya kuja nchini Tanzania,na walivyojaribu kumhamsha hakuamka,walijaribu kumkimbiza hospitali lakin hawakufanikia kwani alikuwa kashafariki,alivyolala akaputiliza kutokana na dozi kuwa kubwa mmno.

Inasemekana kilichosababisha  MAGWEAR kufariki dunia ni kutokana na madawa ya kulevya, nasiku hiyo alizidisha kulala,

MANGWEA atakumbukwa kwa nyimbo zake zilizowahi kutamba kama vile, GETTO LANGU,SPEED 120,MIKASI,NISIKIZE MI,na alikuwa ni kati ya waanzilishi wa kundi la CHEMBE SQUARED ambalo maskani yake yalikuwa mkoani DODOMA, EAST ZOO.

BAADHI YA NYIMBO ZA NGWEAR ZILIZOWAHI KUTAMBA,NA KUPENDWA NA WATU WENGI.



1.MAPENZI GANI,NGWEAR & LADY DEE





2. NGWEAR "SHE GOT GWAIN"





3. TUPO JUU, NGWEAR ft STEVE




4. MIKASI, by NGWEAR ft JAY MO,RAH P





5.NIPENI DILI,NGWEAR ft DARK MASTA



6.NGWEAR, SPEED 120


RIP ABERT MAGWEA

18.5.13

Vugugu la uchaguzi SUA,wagombea tumbo joto....




 Ikiwa ibaki siku moja tuu baada ya wanachuo woote wa sua kuchagua  uongozi mpya, kuongoza kwa kipindi cha muhula mwingine tena wagombea wanaogombea nafasi mbalimbali wakiwa tumbo joto kila mmmoja kuomba ashinde nafasi aliiomba kuchaguliwa.

Hili litawezekana kwa upande mmoja tu wa shilingi kushika hatamu kwa kipindi kingine kinachokuja.

Hapo ikiwa kesho ndio itakuwa siku maalumu kwa wanafunzi woote wa sua kuamua nani atawaongoza katika kipindi kingine cha mwaka mmoja.

Wagombea mbalimbali wamenadi sera zao na leo ndio siku ya mwisho wa kampeni hizo ,hivyo leo ni kampen za lala salama yaani leo(jumamosi,18/05/2013) ndio mwisho kwa kila mdogombea kunadi sera zake.

Nafasi zinanzo gombewa kwa mujibu wa katiba ya Sokone University of Agriculture Students organization
 ( SUASO) ni Rais akiwa pamoja na mmgombea mweza wake(Makamu wa Rais),na wabunge ambao wabunge itakuwa ni baada kupatikana kwa rais na makamu wake.

Wagombea hao ni ANDREW ZIRACK ( Akiwania Urais ) akiwa na mgombea mwenza  SHOO LERNARD (Makamu wa rais), MSEMEMBO BERNARD (akiwania Urais), mgombea mwenza wake ni IRENE MASANGWA (Makamu wa Rais), na GEORGE, LENA (Akiwania Urais) akiwa na mgombea mwenza MSEMO, OBADIA (Makamu wa rais).

Kazi itakuwa kesho kwa kila mwanasua kumchagua mgombea anyefaa kuongoza, maana uchaguzi una sehem kuu mbili kampeni na kuchagua, na kwa tathmini kampen zimeenda vizuri kwa kila mgombea kupata nafasi ya kujinadi kazi kesho ni kila mmoja wetu kwa pamoja tupiga kura kufanya uchaguzi wetu kwa utulivu.

Sababu kumekuwa na mahudhurio machache ya kwa wapiga kura kuhdhuria ktk upigaji kura lakin hili pia ni tatizo la nchi kwa ujumla,wito wangu kwa wanchuo wenzangu kuhudhuria kwa wingi katika zoezi la uchaguzi wa SUASO GORVENMENT LEARDERS.

"TOGETHER WE CAN MAKE CHANGES AT SUA !..............."

11.5.13

UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012


 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012


Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya
Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha
Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka
iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka
aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya. Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba
hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji
wa mitihani hiyo.

Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973
wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika
mwaka uliotangulia.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.
Selestine Gesimba

KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO
YA UFUNDI
10/05/2013

6.5.13

WADAU MBALI MBALI WA MUZIKI WALIVYOONGELEA KUHUSU MGONGANO KATI YA JAY DEE NA RUGE KTK MITANDAO

ON FACE BOOK
228Like ·  · 

Abrahaman Elm J.U.D.I.T.H..W.A.M.B.U.R.A..(J)judith wambura a.k.a. Jaydee you so cute(U)ur star is up dear(D)decission with god love always make you winner&your life always shine(I)ignore fake friends dear(T)tanzania top musician no comm(H)hard work woman_understanding(W)woman of people(A)african natural beutiful woman(M)musoma girl_everyone know(B)bright&innocent woman(U)ur so luck coz you have millions fans(R)road of understanding(A)amazing woman_don't fear_trust your heart_belive in god_luck is yours_wishes are mine dear_best of luck_may god bless you dear!
about an hour ago via mobile · Like · 6


ON TWITTER 

Today was a gudday!! Big Salute to the Queen of Bongo flava. Its a pity the king of Bongo flava is a coward and a snitch!!

3.5.13

NECTA TENA KASHIKASHIKASHI NA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YA 2012,YATAKIWA KURUDIWA TENA





Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu,sera na uratibu bungeni, Msh.William Lukuvi, imetangaza uamuzi wa kupanga upya matokeo ya kidato cha nne ya 2012. Ukitangaza  uamuzi huo mapema leo bungeni na Msh. William Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu. Uamuzi umetokana na kamati ya waziri mkuu iliyokuwa inachunguza kuhusu matokeo hayo kubaini kuwa matokeo hayo yalipangwa kwa utaratibu tofauti na uliokuwa unatumika zamani.

WAKATI hapo awali taarifa zisizo rasmi zilieleza kwamba matokeo hayo yalipangwa kwa kuzingatia madaraja haya hapa chini, japo Baraza la Mitihani lilikanusha baadaye kwa kusema kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli:

A = 80%-100%-
B = 65%-79%-
C = 50%-64%-
D = 35%-49%-
F = 0%-34%-

Wakati huo tume ya Waziri Mkuu imebaini kutumika kwa madaraja tofauti na uataratibu wa awali. Hivyo basi, matokeo yaliyotangazwa hayatatumika tena mpaka yaje yaliyopangwa upya.