3.5.13

NECTA TENA KASHIKASHIKASHI NA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YA 2012,YATAKIWA KURUDIWA TENA





Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu,sera na uratibu bungeni, Msh.William Lukuvi, imetangaza uamuzi wa kupanga upya matokeo ya kidato cha nne ya 2012. Ukitangaza  uamuzi huo mapema leo bungeni na Msh. William Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu. Uamuzi umetokana na kamati ya waziri mkuu iliyokuwa inachunguza kuhusu matokeo hayo kubaini kuwa matokeo hayo yalipangwa kwa utaratibu tofauti na uliokuwa unatumika zamani.

WAKATI hapo awali taarifa zisizo rasmi zilieleza kwamba matokeo hayo yalipangwa kwa kuzingatia madaraja haya hapa chini, japo Baraza la Mitihani lilikanusha baadaye kwa kusema kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli:

A = 80%-100%-
B = 65%-79%-
C = 50%-64%-
D = 35%-49%-
F = 0%-34%-

Wakati huo tume ya Waziri Mkuu imebaini kutumika kwa madaraja tofauti na uataratibu wa awali. Hivyo basi, matokeo yaliyotangazwa hayatatumika tena mpaka yaje yaliyopangwa upya.