28.4.13

TANZANIA INATENGA BILION 1 KILA MWAKA KWAAJIRI YA MAZISHI YA VIONGOZI KITAIFA




Fedha hizo ni zile zilizolalamikiwa na wabunge wakati wa uwasilishwaji wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na ile ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Kutokana na kuwapo mvutano mkali bungeni, kwa nyakati tofauti Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, walilazimika kutoa maelezo ya kina kuwashawishi wabunge wakubali ili fedha hizo ziidhinishwe katika bajeti husika kwa ajili ya matumizi ya mwaka mpya wa fedha unaoanza Juni mwaka huu.

Fedha hizo ni Sh74 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mfuko wa pembejeo, Sh1 bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi wa kitaifa, Sh88 bilioni za Ruzuku ya Mfuko wa Pembejeo na Sh29 bilioni kwa ajili ya kufuatilia utekelezwaji wa miradi ya Serikali.

Baadhi ya wabunge walilalamikia fedha hizo wakisema kuwa ni ulaji kwa wakubwa.

Wakizungumza na gazeti hili, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Tolly Mbwete alisema kwa kuwa Bajeti ya Wizara ya Fedha itapitishwa mwishoni, wabunge wanatakiwa kuikataa hadi mambo muhimu katika bajeti zilizotangulia kusomwa, yatakapofanyiwa kazi.

“Binafsi naona hiyo ndiyo njia nzuri iliyobaki, wabunge wanatakiwa kuamua mambo kwa masilahi ya taifa na siyo kwa manufaa na maslahi yao binafsi,” alisema Profesa Mbwete.

Aliwataka wabunge kutumia fursa hiyo kumbana Waziri wa Fedha ili kuhakikisha kuwa fedha zaidi zinaongezwa, au kupunguzwa katika maeneo mengine, kwa ajili ya kupelekwa katika maendeleo.

Profesa Humphrey Moshi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), alisema kuwa fedha zaidi zinatakiwa kuongezwa katika bajeti ya maendeleo, badala ya matumizi ya kawaida.

Aliongeza pia kwa kusema“Maendeleo yatapatikana kwa haraka kama tutawekeza zaidi ya asilimia 20 ya bajeti yetu kwenye matumizi ya maendeleo. Hii ni tofauti na sasa, ambapo asilimia 90 ya fedha zinazotengwa zinakwenda katika matumizi ya kawaida,” .

umefikia wakati wa Serikali kuachana na matumizi yasiyokuwa na ulazima, kama ununuzi wa samani za ofisiniNaye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Prosper Ngowi aliwataka wabunge kuwa makini na kukubali hoja kwa manufaa ya taifa, siyo kishabiki.