25.11.12

KIVUMBI CHA URAIS 2015 CHADEMA NI BALAA NI ZITO NA SLAA





Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gageti  hili, mpango huo unakuja wakati Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ametangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, kitendo ambacho kiliwashtua vigogo wa chama hicho akiwamo mwasisi wake, Edwin Mtei.
Mtei amekuwa akimwonya Zitto kuwa kitendo chake cha kutangaza nia yake ya kugombea urais kitasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama 
hicho.

Mtei amekuwa akisema kuwa Zitto anatakiwa kuwaunganisha wanaChadema na siyo kuwagawa, au 
kuwavuruga na kwamba siyo shida kuonyesha hisia za kuwania urais, lakini tatizo ni kuwa hali hiyo inatengeneza mzozo mkubwa.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu (BOT) enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Jamii Forum katikati ya wiki hii, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Aliongea na Jamii Forum katikati ya wiki hii, akisema kuwa viongozi wa chama hicho walikutana mjini Morogoro hivi karibuni na kutengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia wanapotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe alisimama kugombea nafasi ya urais akishindana na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akisimama kwa mara ya kwanza.

PIA 2010, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa aligombea nafasi hiyo na kuibuka mshindi wa pili kwa kupata asilimia 26.34 nyuma ya asilimia 61.17ambozo alipata Rais Kikwete.